KOCHA aliyeiwezeha Simba SC kuitoa Zamalek ya Misri na kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2013, Mkenya James Aggrey Siang’a amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Sianga, ambaye hapa Tanzania alizifundisha pia Mtibwa Sugar na Moro United za Morogoro, amefariki dunia usiku wa Saa 6 jana katika hospitali ya Bungoma baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kiongozi wa Kefoca, Bob Oyugi amethibitisha habari za kifo cha Siang’a, ambaye enzi zake alidakia klabu za Gor Mahia, Luo Union na timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars.
“Tumempoteza mtu wetu sana, Siang’a. Mchezaji wa zamani wa kimataifa amefariki ijumaa usiku kwa mujibu wa familia yake. Tunasubiri taarifa zaidi kutoka kwao ili kuendelea na hatua nyingine. Mwili wake upumzishwe kwa amani,” alisema Oyugi.

Mashabiki wa Simba SC watamkumbuka zaidi Sianga baada ya kuipa timu taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati visiwani Zanzibar mwaka 2002, kabla ya kuunda kikosi imara cha vijana wadogo kilichokuwa tishio katika soka ya Tanzania muongo wote huo.
Kikosi hicho kilikuwa kikiundwa na vijana nyota kama, Juma Kaseja, Said Swedi, RamadhaniWasso, Boniface Pawasa, Victor Costa, Lubigisa Madata, Suleiman Matola, Primus Kasonzo, Christopher Alex, Shekhan Rashid, Ulimboka Mwakingwe, Emmanuel Gabriel na Athumani Machuppa.
0 comments:
Post a Comment