Real Madrid wameshindwa kuvunja rekodi ya iliyowekwa na Barca kwenye La Liga ya kushinda mechi 17 mfululizo baada ya kulazimishwa sare na Villarreal katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Madridi ambao ndio walikuwa wenyeji wa mchezo huo walijikuta wakiangukia pua mapema tu kpindi cha kwanza baada ya beki wao Sergio Ramos kuunawa mpira ndani ya boksi na mwamuzi kuamuru ipigwa penati ambay ilifungwa na Bruno Soriano mnamo dakika ya 45.
Sergio Ramos alifuta makosa yake dakika ya 48 baada ya kuisawazishia Madrid bao safi kwa kichwa kutokana na mpira wa kona uliochongwa na James Rodriguez.
kwa muda wote katika kipindi cha pili, vijana hao wa Zinedine Zidane walikuwa wakilisakama lango la wapinzani wao, lakini Villarreal walikuwa makini kuondoa hatari zote.
Kutokana na matokeo hayo, Zidane atabaki kushea rekodi hiyo ya kushinda mechi 16 mfululizo na Pep Guardiola ambaye aliiweka msimu wa 2010-11 alipokuwa akiinoa Barcelona.
Hata hivyo Madrid bado wanabaki kileleni kufuatia kuwa na alama 3 mbele ya Barcelona na 2 mbele ya Sevilla wanaoshika nafasi ya pili.
0 comments:
Post a Comment