Alexis Sanchez ameiokoa Arsebal kupoteza mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya PSG baada ya kufunga goli dakika ya 78 kufuatia kupiga shuti kali lilitokana na kipa wa PSG Alphonse Areola kuokoa mchomo uliopigwa na Alex Iwobi. Mchezo huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Parc des Princes jijini Paris maskani mwa PSG.
Edinson Cavani ndiye alifungua ukurasa wa magoli baada ya kuifungia PSG goli la mapema kabisa mnamo dakika ya 1 kwa kichwa safi na kuipa PSG goli la kuongoza
Kama si uzembe wa Cavani basi leo angeweza kufunga hat-trick kabla ya hata ya kwenda mapumziko lakini kazi nzuri ya David Opsina ilizuia magoli hayo.
Sanchez alipiga shuti lake la kwanza lililolenga lango dakika ya 12 kabla ya mchezo na kuisawazishia Arsenal bao hilo.
Alex Iwobi angeweza kuipatia Arsenal bao la pili lakini mpira uliokolewa na kipa wa PSG.
Olivier Giroud wa Arsenal na Marco Verratti wa PSG walitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kufanyiana vitendo visivyo vya kiuanamichezo.
0 comments:
Post a Comment