Samatta akicheza kwa mara ya kwanza hatua ya makundi ya Europa League akiwa na timu yake ya KRC Genk, ameishuhudia timu yake ikipoteza mchezo wake wa kwanza wa Kundi F kwa kipigo cha ugenini cha magoli 3-2 dhidi ya Rapid Vienna.
Genk walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 29 lililofungwa na Leon Bailey na kudumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili Vienna walitumia dakika tisa pekee kuwa mbele ya Genk kwa magoli 3-1 magoli yaliyofungwa dakika ya 51, 59 na 60.
Dakika za lala salama Genk wakapata penati na Bailey akatupia kambani kuipa Genk bao la pili na kufanya matokeo kuwa 3-2 baada ya dakika 90 kumalizika.
Samatta alianza kwenye kikosi cha kwanza kabla ya kupumzishwa dakika ya 78 kumpisha Nikos Karelis.
Maimamo wa Kundi F baada ya mechi za kwanza za hatua ya makundi Europa League
0 comments:
Post a Comment