Thursday, September 15, 2016

KRC Genk ya Mbwana Samatta leo inashuka uwanjani kuanza kuchanga karata yake mpya kwenye Michuano ya Europa itakapokuwa na kibarua kigumu mbele ya wenyeji Rapid Wien almaarufu Rapid Vienna ya Austria, mchezo wa Kundi F utakaofanyika kwenye Uwanja wa Allianz Stadion.

Kuelekea mchezo huo, Samatta anatajwa kuwa mshambuliaji wa kuchungwa sana kutokana na umahiri wake wa kupachika mabao mpaka sasa msimu huu akiwa ameshapachika mabao sita.

Mabao hayo ya Samatta yametokana na michezo ya Ligi Kuu nchini Ubelgiji na ile ya hatua za awali za kufuzu kucheza Europa. Katika mabao hayo, matatu amefunga kwenye michezo ya ligi na mingine matatu yamepatikana kwenye michezo ya Europa.

Hii si mara ya kwanza kwa KRC Genk na Rapid Vienna kupangwa kwenye kundi moja katika michuano hiyo, kwani walishawahi kukutana tena msimu wa 2013-14

Wakati huo walivyokutana kwenye kundi moja ambalo lilikuwa na timu za Genk, Dynamo Kyiv,  Rapid Wien na FC Thun, Genk walifanikiwa kuongoza kundi baada ya kujizolea pointi 14 wakifautiwa na Dynamo Kyiv waliokuwa na pointi 10, huku Rapid Vienna wakipata pointi 6.

Wakati huo walivyokutana, Genk alishinda mara moja na mchezo mwingine kutoka sare, hivyo kwa rekodi hii, Genk wanaonekana kuwa na faida kubwa zaidi.

Endapo Samatta atafunga leo atazidi kuandika rekodi mpya kwa Tanzania, kwani atakuwa mchezaji wa kwanza Tanzania kufunga goli kwenye mchezo wake wa kwanza kabisa katika Michuano ya Europa.

Kwenye msimamo wa Ligi ya Ubelgiji, Genk wanashika nafasi ya saba wakiwa na pointi 7, huku Rapid Vienna wakishika nafasi ya 4 wakiwa na pointi 13.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video