Real Madrid na Atletico Madrid wameshindwa rufaa zao dhidi ya Fifa juu ya kifungo chao cha kutosajili mchezaji yeyote kwa muda wa miaka miwili.
Vilabu vyote viwili vilikata rufaa juu ya maamuzi ya chombo hicho chenye mamlaka ya juu kabisa kwenye soka duniani baada ya kufungiwa miaka miwili kufuatia kuvunja sheria ya kusajili mchezaji kutoka nje mwenye umri chini ya miaka 18.
Kutokana na hatua hiyo, vilabu hivyo sasa vitaka rufaa kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo.
Atletico wamesema kwamba, tayari wameajiri mtaalam kwaajili ya kushughulikia suala hilo ili klabu yao iondolewe adhabu hiyo.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Fifa Atletico kati ya mwaka 2007 na 2014 Atletico walimchezesha mchezaji mwenye umri chini ya miaka 18, na Real walifanya hivyo kuanzia mwaka 2005-2014.
Vilabu hivyo vimepewa siku 90 ili kuona kama wanaweza kuchukua hatua yoyote.
Atletico walipigwa faini ya francs za Uswisi 900,000 (paundi 622,000), wakati Real waliambiwa walipe 360,000 (paundi 249,000).
0 comments:
Post a Comment