Thursday, September 15, 2016

Licha ya kusubiri mpaka dakika za majeruhi, Mabingwa Watetezi Real Madrid wameanza vyema kampeni yao ya kulitetea taji lao la Champions League baada ya kuwafunga wababe wa Ureno Sporting Lisbon 2-1.

Sporting walianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Bruno Cesar ambaye aliachia shuti kali na kutinga wavuni, lakini Cristiano Ronaldo hakufanya ajizi baada ya kusawazisha mnamo dakika ya 89 kwa mpira wa adhabu ndogo ulioenda moja kwa moja wavuni.

Bao la pili la Real limefungwa na mshambuliaji wao waliomrejesha kutoka Juventus Alvaro Morata dakika ya 90 kwa kichwa. 

Ronaldo alioongeza rekodi yake ya kushindwa kufunga free-kick ya 43 kwenye michuano mikubwa akiwa na Ureno kwenye michuano ya Euro mwaka huu, lakini ameondoa mkosi huo jana kwa kufunga faulo nzuri aliyopiga kutoka takriban umbali wa hatua 25.

Goli hili alililofunga ni la 12 kwa njia ya free-kick tangu aanze kucheza michuano hiyo huku akiwa na rekodi ya kufunga jumla ya mabao 94 kwenye mashindano huku magoli 79 katika michezo 76 akifunga akiwa kama mchezaji wa Real.

Ronaldo sasa anakuwa mchezaji ambaye amefunga kwenye kila mchezo kati ya mitano ambayo alikutana na timu yake ya nyumbani kwenye Michuano ya Champions League.

Alifunga nyumbani na ugenini dhidi ya Sporting wakati akiwa Manchester United mwaka 2007, na alifunga kwenye mechi zote mbili kwenye hatua ya robo fainali fainali ya mwaka 2013 wakati Real Madrid akicheza na MMan United.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video