Dondoo muhimu za mchezo
Head-to-head
- Chelsea hawajapoteza mechi tisa zilizopita za Premier League dhidi ya Arsenal (wameshinda mara sita, droo mara 3).
- Chelsea hawajapoteza mchezo wowote kati ya mitano ya mwisho waliyocheza katika Uwanja wa Emirates (ushindi mara 2, droo mara 3) tangu mara ya mwisho walivyofungwa 3-1 Desemba 2010. Na wameruhusu goli moja tu katika michezo yote hiyo.
- Arsenal wameshinda kupata goli mbele ya Chelsea kwenye mechi sita zilizopita.
- Katika mechi tano za mwisho dhidi ya Chelsea, jumla ya wachezaji wanne wa Arsenal wamejikuta wakitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Arsenal
- Arsenal wanajiandaa kupata ushindi wao wa nne mfululizo kwenye Premier League kwa mara ya kwanza tangu Oktoba mwaka 2015 walivyoweka rekodi ya kushinda mechi tano mfululizo.
- Arsenal wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya 15 iliyopita (wameshinda mara 8, droo mara nne)
- Alexis Sanchez ameshindwa kufunga hata goli moja kwenye michezo minne ya ligi akiwa kwenye Uwanja wa Emirates.
Chelsea
- Kocha wa Chelsea Antonio Conte anaweza kucheza michezo mitatu bila ya ushindi kwa mara ya kwanza tangu mara ya mwisho walivyopata sare nne mfululizo wakati akiwa Juventus Macih 2012.
- Conte hajawahi kupoteza michezo ya ligi mfululizo tangu Desemba 2009 wakati akiwa Atlanta
- Chelsea wamepata clean sheet moja tu kwenye michezo yao ya ligi 12 iliyopita, huku wakiruhusu bao kwenye kila mchezo kati ya michezo sita iliyopita ya ugenini.
- Diego Costa amefunga magoli matano kwenye michezo mitano ya Premier League msimu huu, akifunga kwenye kila mchezo kati ya mitatu iliyopita.
0 comments:
Post a Comment