RAUNDI ya nne ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) itaendelea Mwishoni mwa Juma hili kwa timu zote 16 kushuka Dimbani.
Kesho, Mabingwa watetezi, Yanga SC, watawakaribisha Maji Maji, 'Wanalizombe' kutoka Mkoani Ruvuma.
Yanga wataingia Uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu (0-0) na Ndanda FC katika mechi ya VPL iliyochezwa Jumatano ya Juma hili Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Maji Maji wao wataingia Uwanjani wakiwa na huzuni kubwa ya kupoteza mechi zote 3 za Kwanza na wanaburuza mkia kwenye msimamo.
Mtanange mwingine wa nguvu utawakutanisha Mbeya City FC, 'Wanakoma Kumwanya' dhidi ya makamu Bingwa, Azam FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.
Hapa chini nimekuwekea Ratiba ya Wikiendi hii:
Mpaka sasa timu zote zimecheza raundi tatu kasoro Yanga na JKT Ruvu waliobakiza kiporo chao kilichotakiwa kuchezwa Agosti 31 mwaka huu, lakini kiliahirishwa kutokana na Machampioni hao kuwa na wachezaji 6 kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars, ambacho Septemba 3 Mwaka huu, kilifungwa 1-0 na Nigeria kwenye mechi ya kukamilisha ratiba ya kuwania kufuzu AFCON 2017 nchini Gabon.
Azam FC wanaongoza msimamo wakijikusanyia Pointi 7 baada ya kushinda mechi mbili na kutoka sare moja, huku Mbeya City FC wakiwa nafasi ya pili kwa tofauti ya Mpangalio wa Alphabeti zao kwani wanalingana kwa kila kitu na Wanalambalamba.
Angalia Msimamo hapo chini:
0 comments:
Post a Comment