Kinda wa Manchester United na timu ya taifa ya vijana U21 Marcus Rashford ameng’ara kwenye mchezo wa Kundi la 9 kuwania kufuzu mucheza michuano ya Euro kwa vijana baada ya kupiga hat-trick dhidi ya Norway.
Rashford alianza kupiga bao la kwanza dakika ya 29, Chalobah akafunga bao la pili dakika ya 38 kabla ya timu hizo kwenda mapumziko.
Dakika ya 64 kipindi cha pili Loftus akafunga bao la tatu, Rashford akaendeleza dozi yake dakika mbili baadae kwa kupiga bao lake la pili kwenye mchezo huo, huku likiwa ni la nne kwa timu yake.
Rashford alikamilisha hat-trick yake dakika ya 72 akifunga goli kwa mkwaju wa penati, kisha Baker akakamilisha ushindi wa magoli sita kwa England alipofunga bao mnamo dakika ya 86.
Zahid aliifungia Norway bao pekee la kufutia machozi dakika ya 68 ya mchezo.
Vikosi
England U21: Gunn, Iorfa, Chambers, Hause, Targett, Ward-Prowse, Chalobah, Redmond (Gray, 81), Loftus-Cheek (Watmore, 80), Baker, Rashford (Akpom, 84)
Subs ambazo hazikutumika: Wildsmith, Holding, Hayden, Galloway
Norway U21: Rossbach, Haraldseid, Jenssen, Berge, Grogaard, Elyounoussi (Thorsby, 76), Fossum, Selnaes (Trondsen, 68), Daehli (Zahid, 57), Sorloth, Odegaard
Subs ambazo hazikutumika: Dyngeland, Rosted, Meling, Espejord
0 comments:
Post a Comment