Mwenyekiti wa Yanga SC, Yusuf Manji, ameungana na maelfu ya wadau wa soka, ndugu jamaa na marafiki kuuga mwili wa marehemu Munishi Boniventura ambaye ni baba wa kipa namba moja wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’.
Manji aliungana na wadau hao wa soka, wakiwemo mashabiki, wanachama wa Yanga pamoja na wale wa Simba ambao walijitokeza katika Kanisa Katoliki Temeke Mikoroshini Jana jijini Dar es Salaam.
Baada ya shughuli hizo za kuaga, mwili ulipelekwa kwenye gari na msafara kwenda mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi ukaanza.
Picha zote kwa hisani ya shaffihdauda.co.tz
0 comments:
Post a Comment