Jack Wilshere jana ameichezea kwa mara ya kwanza timu yake mpya ya Bournemouth kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kunako Uwanja wa Vitality maskani mwa Bournemouth.
Katika mchezo hio ambao Wilshere alicheza kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza, Bournemouth walifungwa magoli 2-1.
Goli la Bournemouth lilifungwa na Lys Mousset dakika ya 65, huku magoli ya AC Milan yakifungwa na Suso dakika ya 64 na Mbaye Niang dakika ya 66.
Wilshere ambaye amejiunga na Bournemouth kwa mkopo wa msimu mzima akitokea Arsenal, ameonesha kiwango kizuri licha ya kujiunga na timu hiyo siku ya mwisho kabisa ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya.
Jack Wilshere akipambana na mchezaji wa AC Milan Jose Ernesto Sosa
0 comments:
Post a Comment