Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul amekata nywele zake na kuacha zikiwa ndogo (unga) tofauti na alivyozoeleka kuonekana akiwa ananyoa za pembeni na kuzifuga za katikati ya kichwa.
Kuna wakati mchezaji huyo aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi kuu ya kandanda Tanzania Bara msimu uliopita, aliweka rasta (dread) ikiwa ni moja ya style yake ya nywele.
Lakini kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya Ndanda FC uliochezwa mjini Mtwara, Juma alionekana kwa mara ya kwanza akiwa na nywele fupi kichwa kizima huku akiwa ameachia ndevu kwa mbali kama kawaida yake.
Hizi hapa picha tofauti zikionesha mwonekano mpya wa Juma Abdul.
Picha kwa hisani ya shaffihdauda.co.tz
0 comments:
Post a Comment