Friday, September 9, 2016

 MLINZI mahiri wa Azam FC, Serge Pascal Wawa alikuwa sehemu ya mazoezi ya klabu hiyo Jana Uwanja wa Sokoine wakijiandaa na mechi ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara watakayocheza kesho Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Hata hivyo Wawa na Aggrey Moris ambao ni majeruhi walikuwa na program yao tofauti na wachezaji watakaoweza kucheza.
Nyota hao wawili wanaendelea kuuguza majeraha, lakini mwenzao Fransisco Zekumbawira (Zimbabwe) amerejea kikosini baada ya kupona majeraha yake na huenda akawakabili Mbeya City FC endapo kocha mkuu Zeben Hernandez ataamua.
Haya yalikuwa mazoezi ya kwanza kwa Azam FC tangu waifunge 1-0 Tanzania Prisons Jumatano ya Juma hili na programu hiyo ilikuwa ya kurejesha mwili katika hali yake ya kawaida.
Picha kwa hisani ya Azam FC





0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video