Hans Van Pluijm amewapokea vijana wake waliokuwa nje ya kambi kwa matatizo tofauti, Geofrey Mwashiuya alikuwa majeruhi kwa wiki 6 huku Deogratius Munishi 'Dida[ akirejea baada ya kumaliza mazishi na taratibu za msiba wa baba yake Mzee Boniventura Munishi.
Vijana hawa waliungana na wenzao leo katika mazoezi ya kujiandaa kuwakabili Majimaji hapo kesho Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam.
Yanga wataingia kwenye mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu na Ndanda FC Jumatano ya Wiki hii.
Wakati huo huo, naye naye Mlinzi wa kimataifa wa Yanga SC Vicent Bossou amerejea kuitumikia klabu yake, Bossou ni Mu-ivory Coast ambaye alichukua uraia wa Togo ili kupata nafasi ya kutumikia timu ya Taifa! Togo imefuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika nchini Gabon, Bossou alifunga goli katika ushindi wa 5 - 0 waliopata Togo dhidi ya Djibouti.
0 comments:
Post a Comment