Mapacha wawili wa Simba Ibrahim Ajibu na Laudit Mavugo wameendelea kung'ara katika safu ya ushambuliaji wa timu hiyo baada ya kila mmoja kufunga goli katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Simba ambao walianza mchezo huo kwa kasi kubwa walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Ibrahim Ajibu mnamo dakika ya 53 ya baada ya kuunganisha kona murua iliyochongwa na Shiza kichuya.
Simba waliendeleza mashambulizi kwa kasi ya aina yake na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 65 kupitia kwa Laudit Mavugo na kuzidisha Shangwe kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Kwa matokeo hayo sasa, Simba wamefikisha jumla ya pointi 10 sambamba na Azam ambao wanabaki kileleni kutokana na herufi ya jina lao kutangulia ukilinganisha na Simba.
Matokeo mengine
Prisons 1-0 Toto Africans (Uwanja wa Sokoine)
Matokeo mengine
Prisons 1-0 Toto Africans (Uwanja wa Sokoine)
0 comments:
Post a Comment