Arsenal leo wako nyumbani wakiwa na mtihani mzito watakapokuwa wakiwakaribisha mahasimu wao wa jiji la London Chelsea katika mchezo wa EPL utakaofanyika kunako Uwanja wa Emirates saa 1:30 usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.
Arsenal wanaingia katika mchezo huu wakiwa na imani kubwa kutokana na kuwa na kikosi imara msimu kunzia upande wa safu ya ulinzi mpaka ushambuliaji ukilinganisha na misimu kadhaa iliyopita.
Taarifa muhimu kwa kila timu
Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud leo anaweza kurejea baada ya kukosekana katika michezo miwli iliyopita kutokana na kusmbuliwa na majeraha.
Hata hivyo kiungo Aaron Ramsey bado ataendelea kuwa nje akiunguza jeraha lake la misuli ya paja na kukadiriwa kurudi takriban wiki tatu zijazo.
Kwa upande wa Chelsea, nahodha wao John Terry ataendelea kukosa mchezo wa leo ambao ni mchezo wa tatu mfululizo kufuatia kuendelea na tiba ya jeraha lake la mguu.
Beki mwenzake Mfaransa Kurt Zouma bado ataendelea kubaki nje licha kuwa tayari ameanza mazoezi madogo-madogo.
Kauli za makocha wa timu zote mbili
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger juu ya nidhamu kwa timu yake: "Tumeongea kuhusu hilo kwasababu katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Chelsea tumecheza tukiwa pungufu."
"Hivyo mchezo wa leo utakuwa muhimu sana kwetu kupata matokeo, lakini muhimu zaidi kucheza kwa nidhamu kubwa."
Kocha wa Chelsea Antonio Conte: "Huu ni mchezo mkubwa sana unawakutanisha mahasimu wakubwa. Ni muhimu zaidi kucheza soka safi.
"Zaidi ya hapo baada ya kufungwa na Liverpool kulitufedhehesha. Lakini leo itabidi tupambane sana maana tunafahamu kuwa tunacheza na si tu timu kubwa bali mahasimu wakubwa."
0 comments:
Post a Comment