Wednesday, September 7, 2016

Mechi 5 za Kanda ya nchi za Amerika ya Kusini chini ya usimamizi wa Shirikisho la Soka kwa Nchi za Amerika ya Kusini (CONMEBOL) kusaka mataifa manne yatakayofuzu moja kwa moja kucheza World Cup mwaka 2018 nchini Russia zimepigwa leo kuelekea Alfajiri.

Argentina, ambao walikuwa ugenini bila nahodha wao Lionel Messi anayesumbuliwa na majeraha ya misuli ya paja, walitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Venezuela.

Venezuela ndio walikuwa wa kwanza kupata mabao yao yaliyofungwa dakika za 35 na 53 kupitia kwa  Juan Pablo Añor Acosta 'Juanpi' na Josef Martinez, lakini baadaye kipindi cha pili Argentina walikaza uzi na kusawazisha mambao hayo katika dakika za 58 na 83 kupitia kwa Lucas Pratto na Nicolas Otamendi.

Brazil, wakicheza maskani yao katika Uwanja wa Amazonia Arena, Manaus (Amazonas) waliichapa Colombia 2-1.

Mabao ya Brazil yalifungwa na Miranda, mnamo dakika ya pili huku Neymar akishindilia msumari wa pili mnamo dakika ya 74. Colombia walipata bao la kufutia machozi mnamo dakika ya 36 kupitia kwa beki wa Brazil Marquinhos ambaye alijifunga wakati akiwa katika harakati za kuoko mpira huo.

Kwa upande mwingine Uruguay, wakiwa nyumbani kwao waliichakaza Paraguay bila huruma mabao 4-0. Wafungaji wa mabao hayo walikuwa ni Edinson Cavani (22), Rodriguez na Luis Suarez.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video