Jose Mourinho jana jioni akiwa na wachezaji wake aliwasili katika Hoteli ya Lowry kuelekea'Dabi' kubwa ya leo ya Manchester itayoanza saa nane na nusu mchana kwa saa za Afrika Mashariki.
Mourinho huwa haishiwi vituko, wakati akiingia Hotelini hapo alionekana akikata kucha zake kwa meno zikisalia saa chache kuwakabilia Man City Uwanjani Old Trafford.
Wachezaji wa Manchester United walionekana ku-relax kabisa wakati wanatia miguu Hotelini hapo na hawakupoteza muda baada ya kushuka kwenye basi la timu ambapo waliingia mara moja Hotelini.
Mashabiki wengi wa United walijitokeza Hotelini hapo wakiwasubiri mashujaa wao na waliwapiga picha mbalimbali baadhi ya wachezaji waliokuwa wakiingia Hotelini wakiwemo Zlatan Ibrahimovic, Anthony Martial na Eric Bailly.
Mechi ya leo inarejesha tena upinzani wa Mourinho na Pep Guardiola.
Makocha hao wakubwa waliwahi kuchuana walipokuwa wakizifundisha Real Madrid (Mourinho) na Barcelona (Guardiola).
0 comments:
Post a Comment