Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kesho itakuwa vigumu kuwafunga Manchester City wakiwa bila Sergio Aguero.
Mshambuliaji huyo wa Argentina, 28, amepigwa marufuku kucheza mechi tatu baada ya kumgonga mchezaji wa West Ham,Winston Reid, kwa kiwiko cha mkono mechi ambayo City walishinda 3-1.
Aguero amefunga mabao matatu katika mechi tatu alizocheza Ligi kuu ya kandanda ya England msimu huu lakini Mourinho anasema kutokuwepo kwake kuna maana kwamba City, chini ya Pep Guardiola hawataweza kutabirika.
"Wakiwa na Aguero ni mazingira magumu zaidi, bila Aguero ni vigumu zaidi". amesema Mourinho.
"Pale Aguero anapokuwepo, unajua atacheza, na unajua watajipanga vipi."
"Mchezaji kama yeye (Aguero) anapokuwepo, anacheza. Lakini wana kikosi kipana sana. Anaweza kuwatumia (Kelechi) Iheanacho, (Raheem) Sterling au (David) Silva kama 'nambari tisa bandia' .
Dabi hiyo ya Manchester itakayochezwa kesho uwanjani Old Trafford itaanza saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment