Monday, September 12, 2016

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC, mwishoni mwa Juma hili, (Septemba 17, 2016) walitarajiwa kucheza mechi kali ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Taarifa ambazo MPENJA SPORTS imezipata zinaeleza kuwa Shirikisho la kandanda Tanzania Bara (TFF) limelazimika kuahirisha mechi hiyo na kuipangia tarehe nyingine kwasababu Uwanja wa Taifa utakuwa na matumizi mengine.
Timu ya Taifa ya Soka ya  Tanzania ya Vijana wenye Umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Jumapili ya wiki hii itaivaa Jamhuri ya Congo kwenye mechi ya kwanza ya raundi ya mwisho ya kuwania kufuzu Fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazochezwa Mwakani nchini Madagascar.
Kutokana na kanuni, siku moja kabla ya mtanange, timu ngeni (Congo) inatakiwa kufanya mazoezi Uwanja utakaotumika (Uwanja wa Taifa) na inamaanisha Congo watajifua siku hiyo.
Kutokana na ratiba hiyo, hakutakuwa na nafasi siku ya Jumamosi, hivyo mechi ya Simba imesogezwa mbele.
Hata hivyo, Uwanja wa Uhuru umeshaanza kutumika,lakini haijaelezwa wazi kama hauwezi kuifaa mechi hiyo.
Ripoti za ndani zinadai mchezo huo wa Simba na Azam FC huenda ukachezwa Septemba 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video