Friday, September 9, 2016

Hamad Juma (Aliyelala chini) akijaribu kumdhibiti Laudit Mavugo
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC, wanaendelea kujifua Uwanja wa Boko Veterans Jijini Dar es salaam wakijiandaa na mechi ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara watakayocheza Jumapili hii dhidi ya Wakata Miwa wa Mtibwa Sugar, Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.
Beki wa kulia aliyeanguka bafuni wiki kadhaa zilizopita, Hamad Juma, amerejea mazoezini na jana alionesha kiwango kizuri ambapo alipambana na mshambuliaji hatari wa klabu hiyo, Mrundi, Laudit Mavugo.
Mavugo anayeshika nafasi ya pili kwa upachikaji mabao akiwa amefunga mawili nyuma ya John Bocco mwenye magoli matatu alionesha cheche zake mazoezini kabla ya kuwavaa 'Wana Tam Tam' kutoka Manungu Turiani Mkoani Morogoro. 
 Mavugo (kushoto) akiwapashia Mtibwa Sugar katika mazoezi ya Jana.
 Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' (kulia), Mavugo (katikati) na Nahodha Jonas Mkude wakiwavutia kasi Mtibwa Sugar.
Mpaka sasa Simba wanashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi kuu wakijikusanyia Pointi 7 sawa na Azam FC waliopo nafasi ya kwanza na Mbeya City nafasi ya tatu, lakini wamezidiwa kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Wakali hao wa Msimbazi wameshinda mechi mbili kati ya tatu walizocheza, huku wakitoka sare moja.
Walianza kwa kuwachapa 3-1 Ndanda FC, wakatoka suluhu (0-0) dhidi ya JKT Ruvu na Jumatano ya Juma hili waliibamiza 2-1 Ruvu Shooting.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video