Ligi kuu ya kandanda Tanzania Bara imeenedelea kwa mechi nne kuchezwa ambapo jijini Mwanza, Wenyeji Mbao FC wamekubali kichapo ha mabao manne kwa moja dhidi ya Wanakoma Kumwanya, Mbeya City FC.
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Raphael Alfa aliyetikisha nyavu mara mbili, huku Omary Ramadhan na Ramadhan Chombo.
Bao la kufutia machozi kwa Mbao FC limetiwa kambani na Vicent Philipo.
Huko Kagera, baada ya kutangatanga kwa miaka miwili bila kuwa na Uwanja wa Nyumbani, Wana superNkurukumbi, Kagera Sugar wamezindua uwanja wao wa Kaitaba uliowekwa nyasi bandani kwa kuwachapa bao moja kwa nunge Mwadui FC.
Bao pekee la ushindi kwa Kagera Sugar limefungwa na Ally Ramadhan.
Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvu, Wanalizombe, Maji Maji FC, wamekubali kipigo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya Wakata miwa wa Mtibwa Sugar.
Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Salim Mbonde na Rashid Mandawa, wakati la Maji Maji limeweka nyavuni na Bahati Ngonyani.
Maafande wa JKT Ruvu Stars, wamechuana na African Lyon uwanja wa Mabatini mkoani Pwani na kutoka suluhu.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mchezo mmoja kupigwa ambapo Wenyeji Stand United watakuwa uwanja wa Mwadui kuwavaa Wanakishamapanda, Toto African.
Mechi hiyo imepelekwa Mwadui kwasababu uwanja wao wa Kambarage una matumizi mengine ya kijamii.

0 comments:
Post a Comment