Thursday, September 8, 2016

LIGI kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa Juma hili  na miongoni mwa mechi ngumu ni kati ya Mbeya City FC na Azam FC itayaochezwa Jumamosi Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
City wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na rekodi ya kuongoza ligi kwa mara ya kwanza hivi karibuni na tayari kocha wake, Kinnah Phiri amesema anajipanga vilivyo kuhakikisha timu hiyo haishuki nafasi mbili za juu.

Phiri ambaye yuko na kikosi chake Mbeya  na kilishuhudia mechi ya Jana Sokoine wakati Tanzania Prisons ikilala 1-0 dhidi ya Azam FC, ameleeza kuwa yupo  katika mikakati kabambe itakayoiwezesha timu hiyo kufanya makubwa kwani amekusudia kuweka historia nchini.

“Tunamshukuru Mungu kwa nafasi hii tuliyopo, ni mwanzo mzuri kwetu katika kuhakikisha safari hii tunafanya vizuri katika michuano hii licha ya ushindani kuonekana kuwa mkubwa sana.

“Hata hivyo, hivi sasa nipo katika mikakati kabambe ya kuhakikisha tunaongoza ligi,” alisema Phiri, Raia wa Malawi.

IMG_20160906_133941
Mbeya City wanaendelea na mazoezi Uwanja wa Sokoine, lakini taarifa iliyotolewa na Afisa habari wake, Dismas Ten inaeleza kuwa mshambuliaji Geofrey Mlawa ni wazi ataukosa mchezo wa jumamosi dhidi ya Azam Fc kufuatia majeraha aliyoapata kwenye mchezo dhidi ya Toto African jijini Mwanza na tayari jopo na madaktari wa City wameshathibitisha  jambo hili mbele ya benchi la ufundi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video