Msemaji huyo mwenye mbwembwe nyingi aliongeza kwamba, hii si kwa timu yake tu bali timu yoyote inaweza kucheza vizuri lakini kama bahati haipo kwao siku hiyo, basi ushindi hauwezi kupatikana.
"Nilisema tangu jana kwamba timu inaweza kucheza vizuri, ukawa na uwezo wa kushinda lakini kama bahati haikulalia kwako upande huo, hauwezi ukapata ushindi. Ni bahati ambayo imetufikisha katika matokeo haya ambayo si ya kufurahisha kwa upande wetu," alisema
"Lakini hakika bado tunaendelea na mapambano na bado vijana wana ari, bado timu yetu tuna imani kubwa kwamba tutafanya vyema. Ni mchezo tu wa kwanza huu katika michezo mitatu tumepoteza, hatukupoteza tu kwasababu kwamba uwezo wetu ndiyo umefika hapa,
Bwire alisema kwamba, licha ya kipigo hicho lakini vijana wake walionesha ari na upambanaji mkubwa na kuongeza kuwa anaamini mwalimu ameyaona mapungufu na kuyafanyia kazi ili kuendeleza mapambano kwenye michezo ijao.
"Tumepoteza kama nilivyosema kwamba haikuwa bahati yetu, lakini mpira umeuona vijana wamepambana, vijana wameoesha na hiyo ndiyo staili yetu tutakayokwenda nayo,"
"Haya mapungufu yaliionekana katika Uwanja wa Uhuru hii leo (jana), mwalimu Seleman Mtungwe ameyaona na anakwenda kuyafanyia kazi na nina hakika kwamba marekebisho hayo yatafanyika kwa usahihi na tutakwenda kufanya vizuri,"
0 comments:
Post a Comment