Uhasama mkubwa uliopo kati ya Jose Mourinho na Pep Guardiola na ongezeko la hofu kutokana ukubwa wa mchezo wa Manchester United na City umefanya jeshi la polisi kujipanga namna kuweka ulinzi thabiti kuelekea mchezo huo.
Taarifa za ndani kutoka jeshi hilo zinaeleza kuwa, maofisa wa polisi watakaopangiwa majukumu kwenye mchezo huo wamepewa tahadhari kuwa makini na mokocha hao kutokana na historia ya uhasama wao mkubwa wakati walipokutana miaka ya nyuma.
Takriban maofisa wa pilisi 400 wanatarajiwa kuwa na majukumu mazito ya kuhakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha kwenye mchezo huo huku muda wote wakiwa macho kuwaangalia Mourinho na Guardiola ambao walikuwa mahasimu wakubwa wakati wakiwa katika vilabu vya Real Madrid na Barcelona mtawalia.
0 comments:
Post a Comment