Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yussuf Manji leo ametoa eneo la ekari 715 na kuikabidhi klabu hiyo maeneo ya Kigamboni Geza Ulole jijini Dar es Salaam maalum kwaajili ya ujenzi wa uwanja na wa klabu hiyo.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Waziri wa Mambi ya Ndani, Mwigulu Nchemba, mke wa rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Sheikh Abeid Amaan Karume, Mama Fatma Karume ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu hiyo, ndiye aliyepokea eneo hilo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mama Karume amesema wao kama Baraza la Wadhamini wanashukuru sana kupokea eneo hilo, kwani wanaamini ahadi iliyotolewa na Mwenyekiti wao walipoketi kujdili suala hilo hatimaye imetimizwa.
Yanga wamepata eneo hilo huku mahasimu wao Simba wakiwa katika hatua za ujenzi wa uwanja wao uliopo Bunju.
0 comments:
Post a Comment