Manchester United wameonesha kiwango kibovu kwenye kampeni yao ya ufunguzi wa Michuano ya Euopa ambapo wamejikuta wakipoteza mchezo wao dhidi ya Feyenoord.
Bosi wa United Jose Mourinho amefanya mabadiliko nane kwenye kikosi chake dhidi ya kile kilichocheza na Manchester City na kufungwa 2-1.
Shuti pekee la Anthony Martial ambalo hata hivyo halikulenga lango lango ndilo pekee ambalo United walipiga kwenye kipindi cha kwanza.
Zlatan Ibrahimovic alijaribu bahati yake lakini kichwa chake alichopiga hakikuwa kimelenga lango la wapinzani wao.
Badala yake, Nicolai Jorgensen, ambaye inaelezwa kuwa alikuwa offside, alipiga krosi na kumfikia Tonny Vilhena na kuipa goli pekee la ushindi Feyenoord kuelekea dakika za mwisho.
Ibrahimovic alijaribu tena kuifungia United goli la kusawazisha kwa mkwaju mkali wa free-kick lakini hata hivyo liliokolewa na kipa Brad Jones.
Kwa kipigo hicho, maana yake United wanakuwa wamepoteza michezo minne mfululizo ya ugenini katika Michuano ya Ulaya.
Pogba amezidi kutaabika kwenye eneo la kiungo
Paul Pogba, ambaye alirejea United baada ya kusajili kwa rekodi ya uhamisho iliyovunja rekodi duniani ya paundi mil 89 akitokea Juventus mwezi Agosti, amekuwa akikosolewa kwa ukosefu wake wa nidhamu katika eneo la kiungo na beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher hasa baada ya kipigo cha Jumamosi dhidi ya mahasimu wao Manchester City.
Akiwa amechezeshwa kwa pamoja na viungo kama Ander Herrera na Morgan Schniederlin kwenye eneo la kiungo dhidi ya Feyenoord, Pogba alitakiwa kuonesha uwezo wake mkubwa wa kushambulia, lakini amejikuta amefshindwa kufanya hivyo.
0 comments:
Post a Comment