
Manchester City ambao usiku wa leo waliingiza kikosi kilichokuwa na mabadiliko mengi wamefanikiwa kutinga raundi ya nne ya Kombe la EFL baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Swansea waliokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Gael Clichy ndiye alianza kuifungia City dakika ya 49, likiwa ni goli lake la nne tangu aanze kucheza soka England na baadaye Aleix Garcia kuongeza la pili.
Swansea watajilaumu wenyewe baada ya kupoteza nafasi kufuatia umakini mdogo wa mchezaji wao Borja Baston, kabla ya Gylfi Sigurdsson ambaye aliingia kutokea benchi kufunga goli pekee ambalo hata hivyo halikuwa na msaada wowote.
Nahodha wa Ubelgiji Vincent Kompany alirejea kikosini baada ya kukosekana kwa takribani miezi mitano kutokana na kukabiliwa na majeraha.
0 comments:
Post a Comment