Leicester City wamesherekea kwa mara ya kwanza ushindi kwenye michuano ya klabu Bingwa Ulaya baada ya kuichapa 3-0 Club Brugge ya Ubelgiji .
Marc Albrighton alianza kuifungia Leicester bao la kuongoza kutokana na makosa ya beki wa pembeni Luis Hernandez wa Brugge.
Riyad Mahrez akafunga bao la pili kwa mpira wa adhabu ndogo kabla ya timu kwenda mapumziko.
Mahrez akatupia kambani bao la tatu kwa mkwaju wa penati kufatia Jamie Vardy kuangushwa kwenye eneo la hatari na golikipa wa Brugge Jose Izquierdo.
Kutakuwa na michezo migumu kuliko huu lakini mabingwa hao wa EPL walionesha kiwango kizuri ambacho kinaashiria wanaweza wakafanya jambo kwenye hatua za mwanzoni za ligi ya mabingwa.
Hiyo ilikuwa ni mechi ya tisa kwenye michuano ya Ulaya katika historia ya Lecester huku ukiwa ni ushindi wa kwanza tangu walipopata ushindi dhidi ya Glenavon ya Ireland ya Kaskazini kwenye hatua za awali mwaka 1962-62 wakati klabu bingwa ilikuwa ni kopmbe la washindi.
Kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo Kundi G, FC Porto imetoka sare ya kufungana 1-1 kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya FC Copenhagen of Denmark.
0 comments:
Post a Comment