September 10 Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye amezitembelea ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiwa ni ziara fupi ya kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo utendaji wa shirikisho hilo ambalo linaongoza soka la Bongo.
Katika ziara hiyo, Mh. Nnauye alikutana na Rais wa TFF Jamal Malinzi pamoja na watumishi wengine wa wa TFF, Nnauye ametoa maagizo kadhaa kwa Malinzi kuhakikisha yanatafutiwa ufumbuzi na kutekelezwa.
Maagizo aliyoyatoa Waziri Nnauye ni pamoja na;
Ukaguzi wa kina TFF
Nilimwagiza Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo amtumie mdhibiti na mkaguzi wa mkuu wa serikali afanye ukaguzi wa kina wa rasilimali watu ili tujue ukweli wa mambo ili watanzania waujue halafu ytuondokane na mambo ambayo wakati mwingine hayana msingi.
Kwahiyo utafanyika ukaguzi mkubwa pengine ambao haujawahi kufanyika muda mrefu kuangalia rasilimali fedha na rasilimali watu kuangalia uwezo wa utendaji.
Mishahara ya watumishi
Nimekuwa nikitumiwa message nyingi na watumishi wakidai hawajalipwa mishahara.watumishi wadai wanakaa muda mrefu wakati mwingine miezi mitatu minne hawajalipwa mishahara, manung’uniko yamekuwa mengi.
Rushwa kwenye uchaguzi
Niliahidi kwamba tutasimamia uchaguzi ndani ya TFF uwe uchaguzi wa haki usiogubikwa na matendo ya rushwa ili tupate viongozi wafasi.
Kupitia kikao hiki, nawaagiza TAKUKURU kote waliko, wahakikishe uchaguzi unakuwa wa haki kwa dhibiti vitendo vya rushwa. Kumekuweko na malalamiko mengi sana, sasa kuanzia mikoani wahakikishe uchaguzi unakwenda kwa haki.
Tukikuta mla rushwa tumkamate bila kujali cheo chake wala anatoka wapi, kusiwepo visingizio.nadhani hapa pakibanwa vizuri tutapata viongozi wasafi ambao wameshinda kwa uwezo wao na si kwa pesa zao.
Mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji wa vilabu
Michakato inayoendelea Simba na Yanga na timu nyingine ya kubadilisha mifumo ya uendeshaji. Serikali tunaunga mkono mabadiliko na mijadala. Michakato hii lazima iongozwe isije ikafata shor-tcut, lazima iwe ya uwazi pasiwe na mambo yanayofichwafichwa lazima sheria zifuatwe. Katika hili serikali tutakuwa wakali kwasababu likikosewa litavuruga amani ya nchi.
Thamani ya vilavu hivi inaangaliwa kabla ya mtu hajajipangia bei ya kujinunulia, kujikodishia au kumiliki? Serikali tuko tayari kushirikiana na vilabu kufanya tathmini ya vilabu kabla ya kufikia hatua ya kumilikishana.
Ni vizuri kujua hadhi ya waliokuwa na vilabu hivi kwa miaka yote, wapo wanachama, mashabiki na wapenzi, hadhi na haki zao katika mchakato huu inaangaliwa vipi?
Chanzo: shaffihdauda.co.tz
0 comments:
Post a Comment