Friday, September 9, 2016

Na Mwandishi Wetu, Mbeya
PATACHIMBIKA! Ndivyo hali itakavyokuwa ndani ya Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya, kesho Jumamosi pale Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, itakapokuwa ikisaka pointi tatu muhimu dhidi ya wenyeji wao Mbeya City. Mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Azam FC itaingia dimbani ikiwa na kumbukumbu  ya ushindi dhidi ya Tanzania Prisons (1-0) huku Mbeya City nayo ikitoka kuichapa Mbao ya Mwanza 4-1 katika Uwanja wa CCM, Kirumba Mwanza.
Ubora wa pambano hilo unaongezwa na vita nyingine ya kukaa kileleni, kwani timu zote hizo zina pointi sawa saba kileleni zikifafanana kwa kila kitu, lakini Azam FC ipo juu kutokana na jina lake kutangalia kiherufi. Simba nayo ina pointi kama hizo lakini imezidiwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa (GD).
Ushindi wowote wa Azam FC kesho utaihakikishia nafasi ya kukaa kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya pointi tatu dhidi ya Mbeya City, huku ikiwasubiria wapinzani wake wa karibu Simba, watakaocheza na Mtibwa Sugar Jumapili ijayo (Septemba 11).
Zeben asema ni pointi tatu tu
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, alisema kikosi chake kipo vizuri na anaimani kubwa wataibuka na ushindi mwingine dhidi ya timu hiyo kabla ya kurejea Dar es Salaam.
“Timu iko vizuri na mazoezi yanaendelea vizuri, tumejaribu kufanya tathimini ya mchezo uliopita (Tanzania Prisons) na kufanyia marekebisho kadhaa na  tunaamini kuwa tutapata pointi nyingine tatu kesho,” alisema.
Azam FC itaendelea kuwakosa nyota wake watatu, mabeki Pascal Wawa, Aggrey Morris na mshambuliaji Francisco Zekumbawira, ambao bado wanaendelea na programu za mazoezi mepesi kabla ya kurejea dimbani.
Afurahishwa kuvunja rekodi  
Katika hatua nyingine, Zeben alifurahishwa na baadhi ya rekodi walizofanikiwa kuvunja msimu huu ile ya kutwaa taji la Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga na juzi kuifunga kwa mara ya kwanza Tanzania Prisons (1-0) ndani ya Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Azam FC hadi inatwaa kwa mara ya kwanza taji hilo ilikuwa haijawahi kuifunga Yanga kwenye fainali tatu mfululizo, lakini Zeben ameweza kukiongoza kikosi hicho kulitwaa, vilevile juzi imeifunga kwa mara ya kwanza Prisons jijini Mbeya tokea ipande daraja Julai 27, 2008.
“Benchi zima limefurahishwa kwa kuifunga Yanga na juzi Tanzania Prisons, tunafurahia pia kuisaidia klabu kufikia malengo hayo kwa mara ya kwanza, lakini kwa sasa kilichombele yetu ni mechi ya kesho, Yanga tumeshaachana nayo na pia ya Prisons yameshapita, tunachoangalia ni mchezo wa kesho namna gani tunaweza kuchukua pointi tatu muhimu,” alisema.
Rekodi zao (Head to Head)
Mara ya mwisho kukutana timu hizo msimu uliopita, Azam FC ilipata ushindi kwenye mechi zote mbili, ikianza kwa kuichapa mabao 2-1 katika Uwanja wa Azam Complex kabla ya kuishushia kipigo kikali cha 3-0 ndani ya Uwanja wa Sokoine Februari 20 mwaka huu.
Kitakwimu mpaka sasa kwa mujibu wa rekodi tokea timu hizo zianze kukutana baada ya Mbeya City kupanda daraja mwaka 2013, Azam FC ndio imeonekana kuwa mbabe ikishinda mechi nne kati ya sita walizocheza hadi sasa huku mechi mbili zikienda sare.
Jumla ya mabao 18 yamefungwa ndani ya mechi hizo sita, Azam FC ikifunga robo tatu ya mabao hayo (12) na Mbeya City ikitupia matano tu.
Mechi za kukumbukwa
Mechi pekee zitakazoendelea kukumbukwa tokea timu hizo zianze kukutana ni ile ya Aprili 13, 2014, ambayo Azam FC ilishinda mabao 2-1 na kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ndani ya Uwanja wa Sokoine, ikilibeba kwa mara ya kwanza kihistoria bila kufungwa mchezo hata mmoja.
Pambano lingine ni lile la Novemba 7, 2013, lililofanyika ndani ya dimba la Azam Complex na kuisha kwa sare ya mabao 3-3, huku ikishuhudiwa hat-trick pekee ya mshambuliaji wa Mbeya City, Mwagane Yeya, ambayo bado inasimama mpaka sasa katika mechi walizokutana.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video