Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaanza wikiendi hii ambako katika kundi A, mchezo wa kwanza unapigwa leo Ijumaa Septemba 23, 2016 kwa kuzikutanisha timu za Ashanti United ya Ilala, Dar es Salaam na Pamba ya Mwanza katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Karume jijini.
Kwa mujibu wa ratiba, michezo mingine itachezwa kesho Septemba 24, 2016 kwa kuzikutanisha timu za Lipuli dhidi African Sports utakaofanyika Uwanja wa Kichangani mjini Iringa. Mchezo huo utakuwa ni wa kundi A wakati katika kundi B michezo itakuwa ni kati ya Kurugenzi ya Iringa dhidi ya KMC ya Kinondoni kwenye Uwanja wa Wambi ulioko Mafinga. Mlale JKT itaikaribisha Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Katika kundi C viwanja ambavyo ziko kwenye mabano vitakutaniha michezo kati ya Singida Utd dhidi ya Mgambo Shooting (Namfua), Mvuvumwa na Rhino Rangers (Lake Tanganyika), Polisi Mara na Alliance (Karume, Musoma) wakati Polisi Dodoma itacheza Panone (Jamhuri).
Mechi hizo zitaendelea Jumapili ambako Coastal Union itaialika Polisi Moro (Mkwakwani) itakayocheza na Kimondo dhidi ya Mbeya Warriors (Vwawa). Jumatano Septemba 26, 2016 Mshikamano itacheza na Friends Rangers kwenye Uwanja wa Karume wakati Jumanne kwenye uwnaja huohuo Polisi Dar itacheza na Kiluvya Utd.
0 comments:
Post a Comment