Kipa wa zamani wa Arsemal Jens Lehmann amesema kwamba ameshangazwa sana kuona Arsenal wametumia pesa nyingi kumnunua beki Shkodran Mustafi.
Kwa muda mrefu Arsenal walikuwa mawindoni kutafuta beki wa kati baada ya eneo hilo kuandamwa na majeruhi klabuni hapo.
Na ndipo walipofanikiwa kumsajili Mustafi kutoka Valencia kwa ada ya ya paundi mil £35 kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
"Sio kawaida kuona Arsenal wanasajili beki kwa takriban euro mil 40 - Nimeshangaa sana kwa kweli," alisema. "Nadhani Wenger ni meneja aliyefanikiwa zaidi kwa matumizi bora ya fedha klabuni.
"Mara zote alikuwa anahakikisha timu yake inapata uwakilishi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, ananunua wachezaji wa bei rahisi na kuuza kwa gharama kubwa sana.
"Ni mtu aliyehusika kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha ujenzi wa uwanja mpya na kuhakikisha kuwa kila msimu Arsenal inashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya."
0 comments:
Post a Comment