Jack Wilshere alipoichezea timu yake mpya ya Bournemouth katika mechi ya kirafiki iliyopigwa Alhamisi iliyopita dhidi ya AC Milan |
Arsene Wenger anataka kuanza mazungumzo na Jack Wilshere ya kuongeza mkataba kabla ya mwisho wa mwaka huu kwasababu anamuona kama Nahodha ajaye wa Arsenal na ikiwezekana kuwa kocha wa Gunners.
Arsene Wenger |
'Pengine siku moja atakaa kwenye kiti changu,' amesema Wenger wakati akizungumzia mipango yake yake ya muda mrefu juu ya Wilshere ambaye amempeleka kwa mkopo katika klabu ya Bournemouth, huku kukiwa hakuna kipengele cha kumrudisha katikati ya msimu.
'Ana Ubongo halisia wa soka na anaelewa mpira wa miguu. Unajua, kiuhalisia upo kwenye damu yake'.
'Atatumia maisha yake kwenye mpira. Ni mtu wa mpira, unaweza kuwa unajua hilo au hujui'.
'Namuona akiwepo klabuni hapa baadaye. Nadhani anaweza kuwa mchezaji hapa. Binafsi, natumaini atakaa hapa kwa maisha yake ya soka. Ni mtu halisi wa Arsenal.
Wilshere anatarajia kuichezea Bournemouth mechi ya kwanza leo dhidi ya West Bromwich Albion.
Nyota huyo kwasasa amebakisha miaka miwili kwenye mkataba wake na Arsenal ambao analipwa karibia pauni Elfu 80 kwa wiki.
Washika Bunduki hao wa London wanatarajia kuanza mazungumzo na mchezaji huyo mwenye miaka 24 ambaye alijiunga na Akademi ya Arsenal akiwa na miaka 9.
0 comments:
Post a Comment