Tuesday, September 27, 2016

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wameelekea kisiwani Pemba kuweka kambi maalum kwaajili ya kuwavaa mahasimu wao Simba, mchezo utakaofanyika Oktoba Mosi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo huo kocha wa timu hiyo Mholanzi Hans Van der Pluijm uwepo wao kisiwani humo utawapa fursa nzuri ya kujiandaa kwani kuna utulivu mkubwa utakasaidia kufanya mambo yao vizuri zaidi ikiwa pamoja na kurekebisha makosa yao yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita.

“Pemba kuna utulivu na nafasi nzuri, tunaweza kufanya mambo yetu vizuri na kutafakari. Kuna vitu vya kurekebisha kabla ya kurejea tena kwenye ligi, tutakuwa na muda, hata kama si mrefu sana, lakini tutafanya kila jambo kulingana na muda,” alisema Hans Pluijm.

Ikumbukwe mchezo wa uliopita Yanga wamepoteza dhidi ya Standa United baada ya kufungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Hata hivyo Yanga wana kumbukumbu zuri dhidi ya mahasimu wao msimu uliopita baada ya kushinda michezo yote miwili kwa idadi ya mabao mawili-mawili.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video