Kuelekea pambano la mahasimu wa Jadi kati ya Manchester United na Manchester City, kuna vita kubwa kati ya makocha wawili mahasimu wakubwa Jose Mourinho na Pep Gaurdiola.
Mourinho na Guardiola ni makocha wenye upinzani pindi wanapokutana hasa wakati wakiwa nchini Uhispania, wakati huo Mourinho akiifundisha Real Madrid na Guardiola akiinoa Barcelona.
Sasa kuelekea mchezo huo wenye msisimko wa aina yake kuna matukio kadhaa ya kukumbukwa pindi wawili hawa walipokutana siku za nyuma.
INTER 0-0 BARCELONA | Septemba 2009 | Champions League | Hapo ndipo upinzani wao ulipoanza. Maswahiba hao wawili wa zamani wakati wakiwa Barcelona kwa mara ya kwanza kabisa, walikutana kama wapinzani katika dimba la San Siro kwenye mchezo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa msimu wa 2009-10. Katika mchezo huo Barcelona walitawala kwa kiasi kikubwa lakini wakashindwa kupata goli.
BARCELONA 2-0 INTER | Novemba 2009 | Champions League | magoli ya mapema kabisa kutoka kwa Gerard Pique na Pedro Rodriguez yalimpa Guardiola ushindi wa kwanza dhidi ya mpinzani wake huyo. Hapakuwa na maneno yoyote ya kejeli, lakini ni Xavi tu ndiye alisema: "Tulipata nafasi nyingi sana za kufunga, Inter hawakuwa na kitu."
INTER 3-1 BARCELONA | April 2010 | Champions League | Barca walisafiri mpaka Milan kwaajili ya nusu fainali Champions League dhidi ya Inter Milan. Licha ya kuwa waliwapa ugumu Inter wakati wa michezo ya hatua ya makundi, Wakatalunya hao walijikuta wakitokota na kuchapwa vijana hao wa Mourinho na kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu.
BARCELONA 1-0 INTER | April 2010 | Champions League | Haukuwa mchezo mgumu kwa Mourinho na Inter yake kwani tayari walikuwa na hazina ya mabao 3-1. inter walitumia muda mwingi kucheza mchezo wa kujilinda katika dimba la Camp Nou. Thiago Motta alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi Sergio Busquets. Baada ya hapo Barca waliendelea kutawala mchezo lakini wakafanikiwa kupata bao moja tu lililofungwa na Gerard Pique na kutupwa nje. Mourinho alishangilia mithili ya mtu aliyechanganyikiwa.
BARCELONA 5-0 REAL MADRID | November 2010 | La Liga | Kitendo cha Mourinho la kuwazuia Barca kushinda taji la Champions League kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu akiwa Inter kikampa kazi Real Madrid. Alipewa jukumu madhubuti kwaajili ya kuondoa utawala wa Wakatalunya hao katika La Liga, lakini mwanzo wake haukuwa mzuri. Wakati wakikutana katika mchezo huo Madrid walikuwa hawajafungwa huku wakiwa wanaongoza ligi. Katika mchezo huo, Barcelona walionesha kiwango ambacho kinasemekana ni bora kuwani kutokea kwenye mechi za muda wote za El Classico.
REAL MADRID 1-1 BARCELONA | April 2011 | La Liga | Wakati timu hizi zikikutana, mbio za ubingwa zilikuwa bado zinaendelea. Huu ulikuwa ni mchezo wa El Clasico uliofanyika ndani ya siku 18 baada ya El Clasico nyingine. Mchezo huu ulikuwa mgumu kwasababu kila timu ilikuwa ikisaka nafasi ya kutwaa La Liga, Copa del Rey na vilevile nafasi ya kutinga fainali ya Champions League, ambapo katika mechi zote hizo, timu hizo zilikuwa zinaenda kukutana.
BARCELONA 0-1 REAL MADRID | April 2011 | Copa del Rey | Akiwa katika msimu wake wa kwanza, Mourinho aliipa Real Madrid taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1993 kwa bao pekee lililofungwa kwa kichwa na Cristiano Ronaldo katika muda wa ziada. Iker Casillas aliwanyima kabisa nafasi za kufunga Andres Iniesta na Pedro kwenye kipindi cha pili. Angel Di Maria alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
REAL MADRID 0-2 BARCELONA | April 2011 | Champions League | Huu ulikuwa ni moja ya michezo ya iliyojaa jazba ya kubwa kuwahi kutokea kwa timu zinazofundishwa na Guardiola and Mourinho. Katika mchezo huo Pepe aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa nne wa Real Madrid kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika michezo minne mfululizo za El Clasico, na Mourinho pia alitolelewa kwenye benchi lake. Kutolewa kwa Pepe kuliwapa nafasi nzuri Barca na ndipo Lionel Messi akawawasha mara mbili, huku goli la pili likiwa ni moja ya magoli bora kwenye historia ya Champions League. Kipigo hiko cha Madrid kilipelekea Mourinho kuwakashifu Barca, UEFA na Unicef wakati wa mkutano na wanahabari baada ya mchezo huo.
BARCELONA 1-1 REAL MADRID | May 2011 | Champions League | Huu haukuwa kama mchezo wa awali ambapo Real walilala 2-0. Huu ulikuwa ni mchezo uliokuwa umejaa burudani ya aina yake na usiokuwa na utata wowote. Mourinho hakuwa kwenye benchi la ufundi kutokana na kufungiwa kwenye mchezo wa awali. Aliamua kupanga kikosi kilichokuwa ni 'attacking minded' ili kupata matokeo dhidi ya Barca. Gonzalo Higuain alifunga goli la mapema lakini lilikataliwa kutokana na kufanya madhambi kabla ya bao hilo kupatikana. Pedro aliifungia Barca goli la kuongoza, kabla ya Real kusawazisha kupitia Marcelo licha ya goli licha ya goli hilo kutokuwa na manufaa yoyote kwa timu yake na Barca wakatinga moja kwa moja fainali nyingine ya Champions League.
0 comments:
Post a Comment