MATAJIRI wa Soka la Bongo, Azam FC, wametamba kuwanyamazisha Mbeya City FC 'Wanakoma Kumwanya' katika mechi ya ligi kuu ya kandanda Tanzania Bara itakayochezwa kesho Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Baada ya mazoezi ya mwisho leo Jioni Dimbani Sokoine, Afisa habari wa Wanalambalamba, Jaffar Idd Maganga, ameiambia MPENJA SPORTS kuwa malengo yao ni kuendeleza rekodi ya ushindi.
"Tumejipanga kuhakikisha tunaendeleza rekodi yetu ya Ushindi Uwanja wa Sokoine dhidi ya Mbeya City baada ya kuwafunga msimu uliopita mabao matatu kwa bila". Amesema Jaffar na kuongeza." Tutapambana kesho kuhakikisha tunapata ushindi baada ya kuvunja mwiko kwa Tanzania Prisons katika mchezo uliopita ambao tuliwafunga bao 1-0. Kesho ni zamu ya Mbeya City, wakae mkao wa kula".
"Ushindi dhidi ya Prisons umeleta ari kwa wachezaji na benchi ufundi, kwa maana ya kwamba wachezaji watajituma zaidi kwenye mchezo wa kesho kwa lengo kuondoka na Pointi sita Mbeya".
Jaffar maarufu kwa jina la 'Mbunifu' ameongeza kuwa Wapiganaji wao wako fiti kwa kupigania Pointi tatu licha ya kuwepo kwa majeruhi kadhaa.
"Kikosi kipo vizuri, ukiondoa majeruhi Wawa (Pascal) na Aggrey (Moris) ambao tumekuja nao hapa Mbeya na wanaendelea na mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiweka sawa. Erasto Nyoni pia ni Majeruhi, anasumbuliwa na kidole na amebaki Dar es salaam".
"
Jaffar pia amefafanua kwamba safu yao ya ushambuliaji imezidi kuimarika baada ya Straika Mzimbabwe, Fransisco Zekumbawira kurejea na kufanya mazoezi ya kawaida na kikosi na hapo kesho watamtumia.
0 comments:
Post a Comment