Kesho ndiyo kesho jijini Manchester ambapo mafahari wawili wa jiji hilo Manchester United na Manchester City watakuwa wakikabiliana uso kwa uso mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Old Trafford majira ya saa 8:30 mchana.
Huu unaelezwa kuwa mchezo utakaokuwa na uhasama mkubwa kuwahi kutokea kutokana na uwepo wa makocha wawili ambao pia ni mahasimu wakubwa Jose Mourinho na Pep Guardiola.
Ikumbukwe hawa ni watu waliowahi kufanya kazi kwa pamoja wakiwa Barcelona wakati huo Mourinho akiwa kocha msaidizi wa Louis van Gaal na Pep akiwa mchezaji ambaye alikuwa anaelekea mwishoni.
Wakakutana tena kama mahasimu, Guardiola akiinoa Barcelona na Mourinho akiwa upande wa Real Madrid, na hapa ndipo uhasama wao uliposhika kasi.
Walicheza mechi nyingi zilitoa matokeo tofauti-tofauti, lakini Guardiola akiibuka kinara zaidi.
Angalia jedwali la takwimu zao hapa
0 comments:
Post a Comment