WAKATI Ulimwengu wa Soka ikisubiri kwa hamu 'Dabi' 'Bab kubwa' ya Manchester itakayochezwa kesho Uwanjani Old Trafford kati ya Mahasimu Manchester United na Manchester United Majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki, huku kukiwa na shauku ya ziada ya kuwaona Makocha wapya wa Klabu hizo, Jose Mourinho na Pep Guardiola, wakikwaana kwa mara nyingine, Mourinho ametoa tahadhari kubwa.
Mourinho, ambaye sasa ni Meneja wa Man United, ameonya hatatumbukizwa tena kwenye uhasama wa kupindukia na Guardiola ambaye ni Mkufunzi wa Man City.
Wawili hao walikuwa na upinzani uliojaa vituko na bashasha kubwa huko Spain walipoongoza Timu pinzani wakati Mourinho akiwa Real na Guardiola akiwa Barcelona.
Lakini, kabla ya wote kuwa Makocha Viongozi, Wawili hao walikuwa Timu moja Barcelona, Mourinho akiwa mmoja wa Jopo la Makocha na Guardiola akiwa Mchezaji na kisha kuanza Ukocha.
Wanahabari na Wachambuzi huko Uingereza, na Duniani kote, wamekuwa wakingoja kwa shauku Wawili hao wakikutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza huko England.
Lakini Mourinho amesema kwenye La Liga wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kwa Samaki mmoja mkubwa tu lakini England kuna Papa kila kona.
Ameeleza: “Uzoefu wangu hauniruhusu niwe mpumbavu. Kwa Miaka Miwili mimi na Pep tulikuwa kwenye Ligi ambayo Bingwa nakuwa mimi au yeye, Real Madrid au Barcelona!”
“Kwa hali kama hiyo, kukwaruzana kibinafsi kunaeleweka kwani huweza kubadilisha mambo!”
“Lakini kwenye Ligi Kuu, nikimtilia mkazo yeye na Manchester City, na yeye atie mkazo kwangu na Manchester United, Mtu mwingine atakuwa Bingwa!”
0 comments:
Post a Comment