Jurgen Klopp amemtaja David Silva wa Manchester City kama mchezaji pekee katika Ligi ya England ambaye anamvutia kwa kiasi kikubwa.
Akiongea katika kipindi cha Sky Sports' 'Monday Night Football', Klopp ameweka wazi mapenzi yake kwa mchezaji huyo kutokana na aina ya uchezaji wake.
"Nampenda sana David Silva, ni mchezaji wa aina yake, anazunguka uwanja mzima, ni ana akili nyingi akiwa uwanjani pamoja na mtazamo chanya muda wote," alisema.
"Hata kama sijasikia jina lake likitamkwa sana kufuatia mwanzo mzuri wa klabu yake ya Manchester City kwenye msimu huu wa Ligi ya England, lakini nina uhakika kabisa kazi yake inaonekana na napenda sana ain yake ya uchezaji."
Aliongeza: "Lakini hata hivyo sivutiwi sana na wachezaji wa timu nyingine kwani wana htari kubwa pale unapokutana nao."
Klopp ameanza vizuri msimu huu mpaka sasa akiwa ameshinda michezo minne ikiwemo dhidi ya Arsenal na Chelse ugenini, ametoa sare mara moja na kufungwa mchezo mmoja.
0 comments:
Post a Comment