Timu ya soka ya Tanzania Bara ya wanawake, Kilimanjaro Queens imeanza Michuano ya Kombe la CECAFA kwa kishindo baada ya kuichapa Rwanda mabao 3-, mchezo uliofanyika Uwanja wa Njeru, mjini Jinja, Uganda.
Kilimanjaro Queens walipata mabao yao kupitia kwa Amina Ally pamoja na Asha Rashid aliyefunga mabao mawili.
Rwanda kwa upande wao, walipata mabao yao kupitia kwa Ibangarrye Anne Marrie pamoja na Stumai Abdallah ambaye alijifunga.
Michuano hiyo inashirikisha timu nane ambazo ni wenyeji Uganda, Kenya, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Zanzibar, Sudani Kusini na Tanzania Bara.
Timu hiyo iko chini ya kocha mkuu Sebastian Nkoma katika mashindano hayo ya kwanza kufanyika ukanda huu yakihusisha timu za wanawake.
0 comments:
Post a Comment