Licha ya kucheza kwenye uwanja wa nyumbani, Mbao Fc ya Mwanza imejikuta ikishindwa kuhimili vishindo vya Mbeya City Fc na kukubali kufungwa mabao 4-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliochezwa leo hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.
Mara baada ya mchezo huo kocha wa City Kinnah Phiri, pamoja na mengine mengi lakini pia aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizui kwa kufuata Maelekezo na hatimaye kuibuka na ushindi huo mnono.
“Vijana wangu wamecheza vizuri, wamefanya kazi kwenye kila tulichokuwa tunakifanyia mazoezi, tulijua Mbao wangekuja na mchezo wa kasi kwa sababu walihitaji sana kushinda hasa baada ya kupoteza mchezo wao uliopita, tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kupata pointi saba kwenye michezo yetu mitatu na sasa tunarudi nyumbani kujiandaa na mchzo mwingine”, Phiri alisema.
0 comments:
Post a Comment