
Hat-trick ya Nwankwo Kanu na goli lingine kutoka kwa Robert Pires ulihitimisha ushindi wa mabao 4-1 wa Malegend wa Arsenal dhidi ya Milan Glorie katika mchezo wa ujirani mwema (charity) uliochezwa kwenye Uwanja wa Emirates.
Arsenal walitaka kuanza mchezo wakiwa 12 uwanjani baada ya straika wa zamani wa Nigeria Nwankwo Kanu kuingia uwanjani ilhali alikuwa anatakiwa kuanzia benchi.
Hata hivyo Kanu alifuta makosa yake baada ya kuingia na kufunga goli la kwanza kwa kichwa dakika ya 27 baada ya krosi nzuri kutoka kwa Emmanuel Petit.
AC Milan walisawazisha kupitia kwa Christian Vieri baada ya kufanya juhudi binafsi kabla ya kuukwamisha mpira waavuni.
Kanu alifunga tena goli dakika ya 72 minutes kabla Pires hajafunga la tatu baada ya kuunganisha krosi nzuri ya Fredrik Ljungberg.
Kanu alifunga tena goli lingine la nne kabla ya Vieri kuifungia AC Milan goli la pili na kuhitimisha mchezo huo kwa matokeo ya mabao 4-1.
Mchezo huo ulikuwa maalum kwaajili ya kuchangia kiasi cha euro mil 1 kwenye Foundation ya Arsenal yenya mpango wa kujenga viwanja jijini London, nchini Jordan na Somalia.
0 comments:
Post a Comment