Friday, September 9, 2016

Na Samuel Samuel

Muda mfupi baada ya timu ya Yanga SC kurejea kutoka Mtwara ambako ilitoka 0-0 na Wenyeji, Ndanda FC, Jumatano ya Juma hili, kamati ya mashindano ya Mabingwa hao Watetezi ilituma taarifa kwa benchi la ufundi la klabu hiyo kuwa wameandaliwa chakula cha jioni katika hotel ya Protea. 
Chakula kizuri kwenye hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tatu kiliendana na mazungumzo ya hapa na pale kuwajenga wachezaji kupambana kutetea ubingwa na kujitambulisha rasmi mbele yao baada ya kamati hiyo kuundwa hivi karibu ikiwa na wajumbe 18. 
Young Africans kesho itakuwa na mchezo wake wa tatu wa Ligi kuu dhidi ya Majimaji FC Uwanja wa Uhuru jijini Dar na kamati hiyo ikiwa na wajumbe nguli kama Samwel Lucumay wamewataka wachezaji kujituma zaidi kushinda mchezo huo na ijayo ili kujiweka vizuri kwenye mbio za kusaka ubingwa wa 27. 
Baada ya chakula hicho cha jana usiku , wachezaji walijumuika na kamati hiyo kwa picha za kumbukumbu na maongezi mengine yakiwa siri ya kamati na klabu husika.







0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video