Imekuwa ni kawaida kwa jamii za Kitanzania na hata Afrika kwa ujumla kutoa ushrikiano kwenye masuala ya misiba bila kujali kufahamiana au kutofahamiana.
Hii imekuwa tofauti kwa Simba SC baada ya aliyekuwa kipa wa klabu hiyo Ivo Mapunda kuwarushia tuhuma kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwenye msiba wa kipa Manyika Peter Jr ambaye amefiwa na babu yake hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mapunda ambaye pia aliwahi kucheza Yanga SC na Azam FC ameandika maneno yanayoashiria kuonesha kusikitishwa kwake na tabia hiyo ya viongozi, wanachama na mashabiki wa Simba kutokana na kutojali shida za wachezaji wao.
Mapunda ameenda mbali zaidi kwa kuusifia uongozi wa Yanga kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa wakati wa msiba wa baba wa kipa Deugratius Munishi na kumpongeza Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye alijitokeza hadi kanisani siku hiyo kuungana na Dida na ndugu zake, marafiki pamoja na Wanayanga wengine waliojitokeza.
Zaidi ya hapo Ivo amekumbushia tukio la viongozi wa Simba kushindwa kuhudhuria wakati alipofiwa na wazazi wake ilhali akiwa mchezaji wa timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment