Saturday, September 3, 2016

Taifa Stars leo imehitimisha mchezo wa kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) kwa kuchezea kichapo cha bao 1-0, mchezo wa Kundi G uliochezwa Uyo, Akwa Ibom State.

Katika mchezo huo uliokuwa na kasi kubwa huku Nigeria wakionekana kufanya mashambulizi mengi zaidi, goli pekee la Nigeria lilifungwa na mshambuliaji machachari anayekipiga kunako klabu ya Manchester City Kelechi Iheanacho mnamo dakika ya 79, kufuatia kuachia shuti kali lililomshinda mlinda lango Aishi Salum Manula, ambaye leo alifanya kazi kubwa sana ya kuokoa michomo mingi.

Ihenacho alfinga goli hilo umbali wa mita 25 kutoka langoni mwa Stars baada ya kuanzishiwa na mpira wa kona kabla ya kuusogeza na kupiga shuti hilo.

Kwa matokeo hayo Stars imebaki mkiani na alama 1 baada ya Chad kujitoa huku Nigeria wakiwa na alama 5 na vinara Misri ambao ndio wamefuzu kwenye kundi wakiwa na alama 10.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video