Thursday, September 8, 2016

LIGI kuu Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 inazidi kushika kasi, lakini ushindani unaonekana kuwa mkali ukiangalia rekodi ya ufungaji wa mabao.
IMG- Copy 11
Mpaka sasa mchezaji mmoja tu ndiye amefanikiwa kupachika mabao mawili kwenye mechi moja ambaye ni Raphael Alpha wa Mbeya City FC.

'Wanakoma Kumwanya' Septemba 3 Mwaka huu waliichakaza Mbao FC mabao 4-1 katika mechi ya Ligi kuu iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Alpha alitika kambani mabao mawili kati ya hayo manne, huku mengine yakifungwa na Omary Ramadhan na Ramadhan Chombo 'Redondo'.
IMG-20160903-WA0027
Hata hivyo, Alpha anashika nafasi ya tatu kwa ufungaji magoli licha ya kuwa na idadi sawa na Laudit Mavugo wa Simba SC, kinachosababisha hivyo ni mpangilio wa Alphabeti ya majina yao.

ORODHA YA WAFUNGAJI WATATU WA JUU:

1. John Bocco (Azam FC)-Magoli 3

Agosti 20 Mwaka huu dimbani Azam Complex, Chamazi, Dar es salaam, Straika Mwandamizi,  Bocco alifunga bao moja katika sare ya 1-1 dhidi ya African Lyon. 
Agosti 27, 2016, Azam FC ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Maji Maji FC ya Ruvuma, Bocco alitupia mawili na moja lilifungwa na Mudathiri Yahya.

2. Luudit Mavugo (Simba SC) -Magoli 2

Agosti 20, 2016, Simba ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC, Mavugo alifunga moja ya magoli hayo, mengine yalifungwa na Fredrick Blagnon na Shiza Kichuya.

Septemba 7, 2016, Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam, Mavugo alifunga bao moja kati ya mawili yaliyofungwa na Simba SC katika ushindi wa 2-1 mbele ya Maafande wa Ruvu Shooting. 

3. Raphael Alpha (Mbeya City FC)-Mabao 2

Magoli yote alifunga Septemba 3 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba Mbeya City ikiichaapa 4-1 Mbao FC.




0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video