Kally Ongala amerejea tena kwenye klabu ya Majimaji ya Songea baada ya leo kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuinoa timu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga ambaye msimu uliopita aliifundisha timu hiyo na kuinusuru kushuka daraja, anatarajiwa kuanza mara moja majukumu yake ili kuinusu timu hiyo ambayo mpaka sasa haijashinda hata mchezo mmoja baada ya kucheza michezo sita.
Ongala, ambaye ni mtoto wa marehemu Remmy Ramdhani Mtolo Ongala, pia ameshawahi kuwa kocha msaidizi wa Azam chini ya Marius Omog kabla ya kutimuliwa misimu kadhaa iliyopita.
Ikumbukwe tu katika mchezo wa mwisho wikiendi iliyopita, Majimaji ilipokea kipigo kikubwa cha mabao 4-0 kutoka kwa Simba, mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment