Thursday, September 8, 2016

Crystal Palace wamethibisha kukamilisha dili la kumsajili kiungo wa Arsenal Mathieu Flamini kwa uhamisho huru.

Flamini (32), amekuwa mchezaji huru tangu alipoachwa na Arsenal katika dirisha la kiangazi lililofungwa hivi karibuni, akiwa ameichezea tu hiyo mechi 24 tu msimu uliopita.

Baada ya kukamilisha usajili huo, Flamini alisema: Crystal Palace ni klabu yenye matarajio makubwa ikiwa na wachezaji wazuri na nasubiri kwa hamu kutoa mchango wangu klabuni. Ni changamoto nzuri kwangu na kwa hakika nina furaha kubwa kuwa hapa.

Nimekuwa na wasaa mbalimbali wa kujadili juu ya kujiunga na klabu hii na Alan Pardew na amechangia kwa kiasi kikubwa mimi kufikia maamuzi haya."

Alan Pardew, ambaye hapo awali alionesha dhamira ya wazi kumhitaji kwa mkopo kiungo Jack Wilshere kutoka Arsenal kabla ya kuelekea Bournemouth, amesema: "Nilihisi kulikuwa na umuhimu mkubwa sana kupata mchezaji mwingine kwenye eneo la kiungo. Uwezo wake mkubwa uwanjani utasaidia lakini pia uwezo wake wa kuwa kiongozi uwanjani, kupiga pasi na kukaba utakuwa msaada mkubwa kwa timu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video